Mkataba wa New START kati ya Marekani na Urusi, unaoweka kikomo kwa idadi ya vichwa vya nyuklia pande zote mbili zinapaswa kumiliki, unafikia mwisho wake leo Alhamisi.
Hali hiyo inaziacha Washington na Moscow bila vikwazo juu ya silaha zao za nyuklia na pia inauacha ulimwengu bila mkataba wowote wa kuzuia vita vya nyuklia.
Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa Antonio Guterres amezihimiza Marekani na Urusi kusaini haraka mkataba mpya wa nyuklia, akisema mud awa mkataba wa New START unamalizika katika "wakati mbaya kwa amani na usalama wa kimataifa."
Chanzo; Dw