Kwenye yaliyojiri wiki ndani ya saa 24, Iran na Marekeani mambo bado mazito.
Kuna taarifa kwamba China, Urusi na Iran zimepanga kuungana kwenye mazoezi ya kijeshi ya pamoja ndani ya ghuba ya Oman na mlango bahari wa Hormuz mwanzonı mwa mwezi wa 2.
Mazoezi hayo “yataanza Jumanne katika bandari ya
Chabahar”, iliyoko kusini mashariki mwa Iran kwenye Ghuba ya Oman, shirika la habari la Tasnim lilisema, bila kutaja muda wake.
“Meli za kivita na vyombo vya kijeshi na vya usaidizi vya vikosi vya majini vya China na Urusi, pamoja na meli za kivita za vikosi vya majini vya Iran vya jeshi na Walinzi wa Mapinduzi” zinatarajiwa kushiriki, kulingana na Tasnim.
Mazoezi hayo yatafanyika “kaskazini mwa Bahari ya Hindi” na yanalenga “kuimarisha usalama katika eneo hilo, na kupanua ushirikiano wa pande nyingi kati ya nchi zinazoshiriki”, Tasnim alisema.
Chanzo; Bongo 5