Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mke wa Elon Musk Aishtaki Kampuni ya Mumewe

Ashley St. Clair (27) ambaye ni Mama Mtoto wa Bilionea Elon Musk, ameishtaki Mahakamani Kampuni ya akili mnemba ya xAI ya Grok ambayo inamilikiwa na Elon Musk, akidai kuwa akili mnemba hiyo ilitoa picha zake bandia za ngono bila idhini yake.

Katika Mashtaka aliyowasilisha Jumatano januari 13, 2026 katika Mahakama ya New York, Ashley ameituhumu Grok kuwavua nguo kidigitali, kuwabadilisha na kuwanyanyasa Waathirika wa matukio ya kingono kitendo ambacho kimeifanya Kampuni ya xAI kuthibitisha kuwa Grok haitohariri tena picha za Watu halisi waliovaa mavazi yanayoonyesha sehemu za mwili kwenye mtandao wa kijamii wa X unaomilikiwa na Elon Musk.

Ashley amedai kwamba mwezi huu Grok ilizalisha na kusambaza maudhui mengi ya unyanyasaji wa kingono, ya kimapenzi, na ya kudhalilisha dhidi yake kwa maombi ya Watumiaji hata baada ya kuijulisha Grok hadharani kwamba hakukubali kuvuliwa nguo kwa njia ya kidijitali.

Ashley St. Clair na Elon Musk waliwahi kuwa na uhusiano wa kimapenzi hapo awali ambapo Ashley anadai kuwa wana Mtoto wa kiume aliyezaliwa mwaka 2024.

 

 

 

Chanzo; Millard Ayo

Kuhusiana na mada hii: