Serikali ya Afghanistan imesema imefanikiwa kuzuia jaribio la mashambulizi ya anga dhidi ya Kituo cha kijeshi cha Bagram, kilichokuwa cha Marekani kaskazini mwa mji mkuu Kabul. Mapigano hayo yanatajwa kuwa makali zaidi katika miaka ya hivi karibuni, huku Pakistan ikitangaza kuwa iko katika “vita vya wazi” na Afghanistan ambayo ni jirani yake.
Chanzo; Dw