Milipuko imesikika karibu na makaazi ya rais jijini Ouagadougou, nchini Burkina Faso, na kuzua wasiwasi wa kuwepo kwa jaribio la kumpindua kiongozi wa jeshi Ibrahim Traore.
Milio hiyo ilizua wasiwasi katika jiji hilo, kabla ya serikali kutoa taarifa na kueleza kuwa, magari sita yaliyokuwa na vilipuzi ndio yaliyolipuka karibu na makaazi ya rais.
Hata hivyo, Ofisi ya rais Traore haijazugumzia tukio hilo, wakati huu, kukiwa na wasiwasi miongoni mwa wakuu wa jeshi kuhusu hali ya usalama nchini humo.
Baada ya tukio hilo lililotolea mwishoni mwa juma lililopita, ripoti zinasema kikao cha wakuu wa usalama, kilichokuwa kifanyike jijini Ouagadougou, hakikuendelea kama ilivyopangwa na kuzua maswali kuhusu hali ya usalama nchini humo.
Hayo yanajiri wakati, wanajeshi wa Burkina Faso katika wiki za hivi karibuni wakiendelea kukabiliwa na tishio la mashambulio kutoka kwenye makundi ya kijihadi na kuwepo kwa hofu ya baadhi ya wanajeshi kuuawa.
Chanzo; Nipashe