Israel imetangaza kuwa itaruhusu kufunguliwa kwa sehemu kivuko cha Rafah kati ya Misri na Ukanda wa Gaza, mara tu itakapopata mabaki ya mateka wake wa mwisho anayeaminika kuzikwa Gaza.
Kivuko hicho ni lango muhimu la misaada ya kibinadamu na kilipaswa kufunguliwa chini ya makubaliano ya kusitisha vita ya Oktoba, lakini kimemefungwa licha ya shinikizo la kimataifa.
Marekani imeongeza shinikizo katika siku za karibuni, na Israel imesema uamuzi huo utatekelezwa baada ya wanajeshi wake kukamilisha oparesheni ya kutafuta mwili wa mateka pekee aliesalia Gaza.
Chanzo; Dw