Rais wa zamani wa Ufaransa Nicolas Sarkozy amehukumiwa kifungo cha miaka mitano jela baada ya kupatikana na hatia ya kula njama ya uhalifu katika kesi inayohusiana na mamilioni ya euro ya fedha haramu kutoka kwa kiongozi wa Libya marehemu Kanali Muammar Gaddafi.
Mahakama ya jinai ya Paris ilimuondolea mashtaka mengine yote, ikiwa ni pamoja na rushwa na ufadhili haramu wa kampeni.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya kusikilizwa kwa kesi hiyo mzee huyo mwenye umri wa miaka 70, ambaye alikuwa rais wa Ufaransa kuanzia 2007 hadi 2012, aliitaja hukumu hiyo kuwa "haijazingatiautawala wa sheria".
Sarkozy, ambaye anadai kesi hiyo ina msukumo wa kisiasa, alituhumiwa kutumia fedha kutoka kwa Gaddafi kufadhili kampeni yake ya uchaguzi wa 2007.
Chanzo: Bbc