Kipindi cha televisheni cha Jimmy Kimmel kiliingia hatarini Alhamisi 18,2025 baada kituo cha ABC kuisimamisha show hiyo ya usiku kufuatia maoni yake kuhusu mauaji ya Charlie Kirk, na kuiacha kampuni yao hatarini kibiashara kwani serikali ya Trump inaweza kufanya maisha kuwa magumu kwa mmiliki wa ABC, Walt Disney Co, kulingana na maoni ya mtangazaji wao.
Lakini wanaotetea uhuru wa kujieleza wanasema ni wakati wa kampuni kushikilia msimamo. Kimmel alitoa maoni kadhaa kwenye kipindi chake Jumatatu na Jumanne kuhusu jinsi watu walivyoyapokea mauaji ya mwanaharakati wa siasa Charlie Kirk, akidokeza kuwa wafuasi wengi wa Trump wanajaribu kutumia kifo cha Kirk kwa faida yao.
"Wafuasi wa MAGA wanajaribu kumkana kijana aliyemuua Charlie Kirk kama mtu asiyekuwa mmoja wao na kufanya kila wawezalo kupata faida za kisiasa kutokana nayo" alisema Kimmel.
Mwenyekiti wa Tume ya Mawasiliano ya Shirikisho, Brendan Carr, alisema Kimmel amefanya makusudi kuwapotosha watu kuwa mtu anayeshtakiwa kwa mauaji hayo alikuwa mfuasi wa Trump wa mrengo wa kulia. Mamlaka inasema Tyler Robinson, mwenye umri wa miaka 22, alilelewa katika familia ya kihafidhina kusini mwa Utah lakini alikuwa ameingia katika "mawazo ya mrengo wa kushoto."
Chanzo; Tanzania Journal