Mwanamke mmoja kutoka Saudi Arabia ameripotiwa kumpa figo mke mwenza wake, katika hatua ya kiutu na ya kushangaza kwa wengi.
Mwanamke huyo, Noura Salem Al Shammari, mke wa kwanza wa Majed Baldah Al Roqi, kwa muda muda mrefu alimuona mke mwenza wake akidhoofika kiafya kutokana na ugonjwa wa figo na matibabu ya mara kwa mara ya kusafisha damu.
Kama ishara ya upendo na huruma, Noura aliamua kutoa figo yake kwa mke mwenza, uamuzi ulioibua hisia kali na mjadala mpana kuhusu mahusiano ya wake wenza.
Uamuzi wa mwanamke huyo unachukuliwa kama uliovuka mipaka ya kawaida ya uhusiano wa ndoa na kuonyesha kuwa utu unaweza kushinda changamoto za kihisia na kijamii.
Chanzo: Dw