Jeshi la Nigeria limesema wanamgambo wameshambulia kambi ya kijeshi iliyopo katika jimbo la Borno, kaskazini mwa nchi hiyo.
Wanajeshi na wanamgambo kumi na mmoja wameuawa katika shambulizi hilo. Jeshi limesema washambuliaji walitumia droni kushambulia kambi ya Sabon Gari.
Msemaji wa Jeshi la Nigeria amesema wameshuhudia kuongezeka kwa matumizi ya droni katika mashambulizi yanayofanywa na waasi.
Chanzo; Itv