Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya (DCEA) imeeleza kuwa, mtaa wa Wailes, Temeke, Dar es Salaam, zimekamatwa pakiti 20 za skanka zenye uzito wa kilogramu 20.03 zikiwa zimefichwa ndani ya balo la mitumba na kufichwa kwenye bus aina ya Scania la Kampuni ya King Masai Tours, lenye namba za usajili wa nchi ya Msumbiji namba AAM 297 CA.
Bus hilo hufanya safari zake kati ya Nampula nchini Msumbiji na Tanzania.
Watuhumiwa waliokamatwa kuhusiana na tukio hilo ni Amasha lddi Mrisho (40), mkazi wa Buza, Dar es Salaam na Seleman Juma Ally (32), raia wa Msumbiji.
Chanzo; Itv