Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

TRA,Wafanyabiashara Wanaohangaika Kufuta Madeni Wakanywa

Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), Yusuph Mwenda amewaonya wafanyabiashara wanaodanganywa na madalali kuwa watawafutia madeni ya kodi na kuwataka kufika kwenye ofisi za mamlaka hiyo kama wanachangamoto.

Kamishna Mwenda amesema kwa kawaida deni la kodi halifutiki mpaka mhusika anapoamua kulilipa au kulipinga na kushinda kesi mahakamani.

Aliyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akizindua Kituo cha Huduma kwa Wateja eneo la Masaki Kinondoni jijini Dar es Salaam, kituo ambacho kinatarajiwa kuwahudumia zaidi ya walipa kodi 6,000.

Amesema kuna baadhi ya wafanyabiashara wenye madeni ambao wanadhani kuwa wanaweza kufanya mchezo kwa kuwatumia watu wa mitaani na madeni yakafutika hali aliyoielezea kuwa ni kujidanganya na kupoteza muda wao.

“Nataka niwaambie wafanyabiashara tena wa nchi nzima kuwa kodi haifutiki isipokuwa kwa mambo mawili tu, aidha umeilipa au umeipinga ukaenda mahakamani na mahakama ikasema vinginevyo lakini nje ya hapo utadanganywa tukikugundua utalipa gharama mara mbili utalipa kodi yenyewe na faini,” amesema

Amesema mfanyabiashara yeyote mwenye changamoto ya kikodi anapaswwa kufika kwenye mamlaka hiyo kupata ushauri kwa wahusika badala ya kuhangaika na watu wa mitaani wasiokuwa na ujuzi wa kodi.

Amesema wafanyabiashara pia wanaweza kuwatumia washauri wa kodi ambao wamesajiliwa kisheria kufanya kazi hiyo badala ya kutafuta njia za mkato mkato kwa watu wa mitaani.

“Unaweza kupata ugonjwa wa moyo kwa kudanganywa, ukiwa na deni la kodi dawa ni moja tu kulilipa kwa wakati na kwa usahihi, kodi ikisimamiwa vizuri kunakuwa na usawa, mwenye kipato kidogo wanalipa kidogo na wenye kipato kikubwa walipe kikubwa,” amesema Mwenda

Aidha, amesema kuna baadhi ya wafanyabiashara wanaamini kuwa wafanyabiashara wakubwa hawalipi kodi wanayostahili kama wale wadogo.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: