Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na Mbunge wa Jimbo la Arusha Mjini, Paul Makonda, leo Februari 3, 2026, amefanya ziara ya kikazi mkoani Arusha, akitembelea miradi mbalimbali ya maendeleo ikiwamo ujenzi wa Stendi ya Mabasi ya Arusha.
Katika ziara hiyo, aliyoambatana na Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amos Makalla, pamoja na viongozi wengine, mbunge huyo amesema mradi wa stendi hiyo umekuwa ukijadiliwa kwa miaka mingi bila utekelezaji wa vitendo.
Ameeleza kuwa sasa amehakikisha mradi unaanza kutekelezwa ili kutatua changamoto za usafiri na biashara jijini humo.
Amesema ujenzi wa stendi hiyo utatoa fursa za kiuchumi kwa wananchi, kuboresha mazingira ya biashara kwa wafanyabiashara na watoa huduma za usafiri, pamoja na kuongeza mapato ya Halmashauri.
“Chini ya usimamizi wako, Mkuu wa Mkoa, sina mashaka kuwa mkandarasi huyu atafanya kazi kwa bidii na kuikamilisha kwa wakati, ili kabla ya AFCON, mheshimiwa Rais aje atuzindulie stendi yetu.
Stendi hii inapojengwa ni fursa ya uchumi inayoletwa hapa,” amesema.
Chanzo; Global Publishers