Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanahabari wa Mitandao ya Kijamii Tanzania (JUMIKITA) Shaban Omary Matwebe, amempongeza Waziri wa Habari, Sanaa, Utamaduni na Michezo Paul Makonda kwa kuamua kupambana kwa ajili ya kuhakikisha vijana waliojiajiri kwenye sekta ya habari za mitandaoni wanapata mikopo itakayowawezesha kununua vifaa vya kisasa.
Aidha, Ndugu Matwebe amemuomba Makonda kuhakikisha anapambana ili mitandao ya Instagram na TikTok pia waanze kuwalipa watumiaji wake nchini Tanzania kama ilivyo kwa nchi nyingine.
Chanzo; Itv