Mfululizo wa matukio unaendelea dhidi ya mwanasiasa na mwanaharakati Humphrey Polepole, tangu taarifa za kutekwa kwake zianze kunea Oktoba 6,2025.
Gumzo lilizidi kutanda mara baada ya Jeshi la Polisi, kusema Polepole bado anatakiwa kuripoti kituo cha Polisi hivyo taarifa za kutekwa kwake zinafanyiwa kazi. Oktoba 7,2025 taarifa kubwa dhidi ya ya mwanasiasa huyo ni kutoweka kwa mitandao yake ya kijamii ya Facebook na Instagram jambo ambalo linazidi kuibua maswali mengi dhidi yake “Yupo wapi Polepole ?
Lingine ni, Kaka wa Humphrey Polepole, Agustino Polepole, anatafutwa na Jeshi la Polisi kwa ushirikiano na atoe uthibitisho wake kuwa waliohusika na tukio kama ni Jeshi la Polisi.
Chanzo: Tanzania Journal