Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wadakwa kwa Kudukua Mfumo wa Malipo Simu za Mkopo

Jeshi la Polisi mkoani Mbeya limewakamata watu wawili, Charles Oden maarufu Mwakasege (32) na Isack Charles maarufu Bebwa,wakidaiwa kuingilia mifumo ya makampuni ya kukopesha simu.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, SACP Benjamin Kuzaga,amesema walikamatwa kwenye msako maalum uliofanyika Januari 27 hadi Februari 5, mwaka huu, ni wakazi wa Mbeya.

“Inadaiwa walikuwa wakibadili simu za mkopo na kuondoa mifumo ya ufuatiliaji, ili kukwepa ulipaji. Polisi walikuta wakiwa na simu mbalimbali pamoja na vifaa vya kufuta taarifa na kompyuta mpakato.

“Uchunguzi wa awali umebaini baadhi ya simu hizo ni za mkopo, huku nyingine zikiwa za wizi zimeibiwa,” amesema.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: