Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mwili wa Joshua Wawasilia Tanzania Ukitokea Israel

Mwili wa Kijana Joshua Mollel aliyeuawa nchini Israel na wapiganaji wa HAMAS Oktoba 07, 2023 umewasili leo Novemba 19, 2025 katika Uwanja cha Ndege cha kimataifa wa Kilimanjaro (KIA) Wilayani Hai Mkoani Kilimanjaro.

Mabaki ya Mwili wa marehemu Joshua Mollel yamewasili saa nane kasorobo na kupokelewa na Nabu Katibu Mkuu Wizara ya Mambo ya nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki balozi Said Shaib Mussa ,Balozi Silima Haji Kombo na mkuu wa wilaya ya Simanjiro Fakii Lulandala.

Mwili wa Kijana Joshua Mollel unatarajiwa kuzikwa Novemba 20, 2025, katika mtaa wa Njiro kata ya Orkesumet wilayani Simanjiro, Mkoani Manyara. 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: