Mbunge Mteule wa Jimbo la Ilala, Dar es Salaam, Mussa Azzan Zungu ameapa rasmi kuliongoza Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama Spika wa Tisa wa Bunge la 13, katika hafla iliyofanyika leo Novemba 11, 2025, jijini Dodoma.
Kiapo hicho kinaashiria rasmi kuanza kwa majukumu yake mapya ya kuliongoza Bunge hilo kwa kipindi kijacho cha miaka mitano.
Zungu ambaye amekuwa Mbunge kwa miaka 20 tangu mwaka 2005 amewahi kushika nyadhifa mbalimbali ikiwemo Mwenyekiti wa Bunge kati ya mwaka 2012 hadi 2021 na Naibu Spika kuanzia 2022 hadi 2025 na ana elimu ya Uhandisi wa Ndege aliyosomea Tanzania na Canada pamoja na shahada katika masuala ya Diplomasia alizohitimu mwaka 2007 na 2021.
Chanzo; Millard Ayo