Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Polisi Washangaa Taarifa za Mchungaji Kutekwa

Jeshi la Polisi limesema linashangazwa na taarifa za Mchungaji Yanick Mbombo Cele raia wa Kongo, kutekwa na watu wasiojulikana jijini Dar es Salaam.

Taarifa ya Polisi iliyosainiwa na Msemaji wa Jeshi hilo, imeeleza kuwa Yanick Mbombo ambaye alishawahi kuwa Mchungaji Kiongozi wa Kanisa la Ebenezer Restoration Ministry for all Nations, Mei 15, 2025 alikamatwa mkoani Iringa kwa tuhuma za ubakaji na mauaji ya watoto wadogo.

Uchunguzi pia ulibaini Mchungaji alikuwa akiishi nchini kinyume cha sheria, Juni 17, 2025 Mchungaji pamoja na wenzake watano walifikishwa Mahakamani na kusomewa mashtaka ya kuendesha genge la uhalifu na kujipatia kesi kwa njia za udanganyifu kesi namba ECO 00014959/2025, ushahidi wa kesi ya mauaji na ubakaji haukujitosheleza hivyo hakuandaliwa mashtaka.

Julai 14, 2025 hukumu ilitolewa na watuhumiwa walikiri kosa kwa njia ya Plea bargain, walilipa faini ya shilingi milioni 20 kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na magari yao yakataifishwa.

Baada ya hukumu hiyo ilibainika bado Mchungaji Yanick anaendeleza udanganyifu kupitia kanisa lake la Ebenezer Restoration Ministry for all Nations, alikamatwa tena na Ofisi ya Mkuu wa Upelelezi Iringa ikamkabidhi kwa Kamanda wa Uhamiaji Mkoa wa Iringa, ambapo Mchungaji huyo aliondolewa nchini na hakutakiwa kurudi tena.

Jeshi la Polisi limeshangazwa kuona taarifa kwenye mitandao ya kijamii kuwa Mchungaji huyo alikuwepo nchini na ametekwa.

Baada ya kuiona taarifa hiyo Jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na linaomba yeyote mwenye taarifa au ushuhuda utakaowezesha kuthibitisha taarifa hizo awasilishe kwenye kituo chochote cha Polisi karibu naye.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: