Mara, Butiama, Ibrahim Shida (24) mkazi wa Sirorisimba anatuhumiwa kumua mke wake Tatu Marwa (25) mkazi wa Sirorisimba kwa kumchoma kisu maeneo ya shingoni.
Taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoani humo inasema Ibrahimu alitekeleza tukio hilo September 12,2025, usiku na mara baada ya kutekeleza tukio hilo aliamua kujichoma kisu shingoni na kufariki dunia njiani akipelekwa hospitali.
Aidha, Jeshi la Polisi linatoa wito kwa wananachi wanapokuwa na changamoto za kifamilia, matatizo ya kiakolojia wasite kuwasilisha wazazi, wiongozi wa dini na wazee wa jadi ili kupata msaada mapema na kuepusha madhara makubwa.
Chanzo: Tanzania Journal