Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Serikali imeunda tume maalum kuchunguza matukio ya Oktoba 29 siku ya uchaguzi mkuu, hatua inayolenga kubaini chanzo cha changamoto zilizojitokeza na kutumia matokeo ya uchunguzi huo kama mwongozo wa kuimarisha mazungumzo ya amani na utulivu nchini.
Rais Dkt. Samia Suluhu Hassan, ametoa kauli hiyo wakati akilihutubia Bunge la 13 jijini Dodoma katika hafla ya kulizindua rasmi Bunge na akisisitiza kuwa uchunguzi huo ni sehemu ya dhamira ya Serikali kuhakikisha unajua chanzo cha Vurugu hizo.
Chanzo; Clouds Media