Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wanaohifadhi Fedha Kwenye Matiti, Pindo la Kanga Chanzo Ubora Kupungua

Benki Kuu ya Tanzania (BoT) imewakataza wananchi, hususan kina mama, kuhifadhi fedha kwenye matiti ikieleza tabia hiyo huharibu ubora wa fedha na kuilazimisha Serikali kugharamia kuchapisha mpya kabla ya muda wake wa matumizi kuisha.

Mbali na kuhifadhi kwenye matiti, kufunga fedha kwenye pembe za kanga au vitambaa hali hiyo inasababisha fedha kujikunja na kuchakaa.

Kauli hiyo imetolewa jana Januari, Januari 25, 2026 na Ofisa Mwandamizi Mkuu wa Kurugenzi ya Mifumo ya Malipo ya Taifa, Kidee Mshihiri, wakati akizungumza na waandishi wa habari katika maadhimisho ya wiki ya huduma za fedha kitaifa, yatakayofikia tamati kesho.

Mshihiri amesema endapo tabia ya kuhifadhi fedha kwenye matiti itaendelea, nyingi zitaharibika mapema hali itakayoongeza mzigo kwa Serikali kugharamia uchapishaji badala ya kuelekeza rasilimali hizo kwenye sekta muhimu za maendeleo.

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: