Ingawa mara nyingi harusi ni tukio linalofurahiwa na kusherehekewa, hali imekuwa tofauti kwa Zainab Kombo, aliyefanya sherehe baada ya kupewa talaka na aliyekuwa mume wake.
Hatua ya Zainab imeibua mitazamo tofauti kutoka kwa wadau wa maadili, wataalamu wa sosholojia, viongozi wa kiroho na Serikali, baadhi wakimuunga mkono, huku wengine wakimpinga.
Viongozi wa dini wao wanasema sherehe za talaka zinapaswa kupingwa kwa sababu hazitoi mfano mwema kwa jamii na zinavunja heshima iliyopewa taasisi ya ndoa.
Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalumu, Dk Dorothy Gwajima, anasema hata kwake tukio hilo limekuwa jambo geni.
Chanzo; Mwananchi