"Mkoa wa Dar es Salaam unaongoza kwa matumizi ya mkaa Tanzania. Unaweza ukajaribu kujiuliza kwa mfano kwa mwananchi wa Dar es Salaam ambaye bado yupo hapa Jijini na anatumia mkaa kupikia, unaweza ukaona kwamba sio suala tu la kiuchumi pia ni watu kutokuwa na ule uwelewa au fikra ambazo wametoka nazo toka huko kutokana na zile jadi au tamaduni ambazo tumekuwa nazo.
"Na tunahitaji kuwabadilisha hawa watu taratibu na pia ni elimu ambayo tunahitaji kuwapa watu na kuwaonyesha faida ya matumizi ya nishati safi ya kupikia"- Benezeth Kabunduguru ( Mhandisi Nishati safi ya kupikia)
Chanzo; Clouds Media