Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Shabiby Adai Tanzania Kuna Mafisadi Wanakula Kuliko Inavyodhaniwa

Mbunge wa Gairo (CCM), Ahmed Shabiby, ameliambia Bunge kuwa Tanzania bado ina mafisadi wengi, akidai kuwa kiwango cha ufisadi ni kikubwa zaidi kuliko inavyodhaniwa na wananchi.

Ametoa kauli hiyo bungeni leo Jumatano, Januari 28, 2026, wakati akichangia hotuba ya Rais Samia Suluhu Hassan aliyotoa Novemba 14, 2025 wakati wa uzinduzi wa Bunge. Shabiby amesema Rais alisisitiza kuundwa kwa Serikali yenye uwajibikaji na inayowatumikia wananchi ili hatimaye kuleta tabasamu kwa Watanzania.

“Kuna mafisadi wengi tena wakubwa. Watu wanajenga nyumba kila kukicha, wengine wanaandika hata majina yao kwenye nyumba. Hivi hili hamlioni au mnataka nani aseme? Wananchi wanaona,” amesema Shabiby.

Ameeleza kuwa vitendo vya ufisadi vinafanyika waziwazi huku akihoji ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya wahusika. Ameikosoa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), kwa madai ya kuwaacha wenye mamlaka na kuwakimbiza wabunge wasiokuwa na fedha za Serikali.

“Watu wa maadili wako wapi? Wanakuja kutufuata sisi wabunge ambao hatuna fedha za Serikali, lakini wanawaacha mawaziri ambao ndiyo wanaoshika fedha za Serikali,” amesema.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: