Mwanaume mmoja aliyefahamika kwa Jina la Bendera, Mkazi wa Mtaa wa Kambi ya Chupa Kata ya Baraa Jijini Arusha, anadaiwa kujitoa uhai kwa kujinyonga akiwa nyumbani kwake na Mke wake huku chanzo kikiwa hakifahamiki.
Majirani wa Marehemu wamesema Mke huyo aliwaita Majirani na kuwaambia kuwa akiwa bafuni anaoga alisikia kishindo chumbani na alipofika alimkuta Mume wake akiwa ameshajinyonga.
Askari wa Jeshi la Polisi walifika eneo la tukio na kuuchukua mwili wa Marehemu Bendera.
Chanzo: Millard Ayo