Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mapya Yaibuka Kesi ACT Wazalendo Dhidi ya ZEC

Dosari ya kisheria inayomhusisha wakili aliyesaini viapo vinavyohusu kesi iliyofunguliwa na Chama cha ACT Wazalendo kupinga hatua ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ya kuteketeza nyaraka maalumu za uchaguzi imesababisha iahirishwe.

Imeelezwa kuwa viapo hivyo vilivyowasilishwa mahakamani, wakili Usi Khamis Haji, ambaye hakuwa na leseni halali ya uwakili kwa wakati husika.

Jaji wa Mahakama Kuu ya Zanzibar, Salma Ali Khamis, aliahirisha kutoa uamuzi wa kesi hiyo leo Febuari 10 Mahakama kuu Tunguu, hadi itakapotajwa Tena Februari 13 mwaka huu.

Katika kikao cha kesi hiyo, Mahakama ilielezwa kuwa viapo vilivyowasilishwa na upande wa walalamikaji, vilisainiwa na wakili huyo bila kuwa na sifa za kisheria, jambo lililoibua hoja nzito ya kisheria iliyolazimu Mahakama kuahirisha kesi hiyo.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: