Baraza la Maaskofu Katoliki Tanzania (TEC), Kupitia kwa Rais wa Baraza hilo na Askofu wa Jimbo Katoliki la Lindi, Mhashamu Wolfgang Pisa, limesema imethibitika kuwa baadhi ya waliopoteza maisha, miili yao haijapatikana na kwamba inasikitisha ya kuwa baadhi ya Watu walipotaka kuwazika wapendwa wao hawakuikuta miili yao.
TEC imeomba kama Wadau wengine walivyokwisha omba kuwa ni hekima na busara kuwapatia wanafamilia miili ya wapendwa wao wakaipumzishe au kuisitiri kwa heshima kadiri ya imani ya dini, mila, desturi na tamaduni zao.
“Imani yetu inatufundisha kuwa kuna maisha baada ya kifo na kifo ni kuanza maisha mapya na pia miili hii itafufuliwa siku ya mwisho maana parapanda italia wafu watafufuliwa
wasiwe na uharibifu nasi tutabadilika (1 Kor. 15:52)."
Chanzo; Millard Ayo