Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Vijana Waonywa Matumizi Madawa ya Kulevya

Waziri Mkuu, Dk. Mwigulu Nchemba, amewataka vijana kujiepusha na matumizi na biashara ya dawa za kulevya, akisema tabia hiyo ni tishio kwa mustakabali wao na maendeleo ya Taifa.

Ujumbe huo umetolewa kwa niaba yake na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka, leo Februari 4 wakati wa kongamano la kimataifa lililofanyika katika Chuo Kikuu cha Jordan mkoani Morogoro.

Nanauka amesema Afrika ya kesho inahitaji vijana wenye afya njema, maadili mema na maono ya maendeleo ili waweze kushiriki kikamilifu katika ujenzi wa taifa.

Kongamano hilo liliandaliwa na Portable Practical Education Preparation (PPEP) kwa kushirikiana na vyuo vikuu na taasisi mbalimbali za ndani na nje ya nchi chini ya kaulimbiu isemayo 'Afrika ya Kesho'.

 

 

Chanzo; Nipashe

Kuhusiana na mada hii: