Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mtoto Akutwa Amefariki Baada ya Kupotea Siku 6

Mtoto wa kike mwenye umri wa miaka saba (7) anayefahamika kwa jina la Magreth Dickson mwanafunzi wa darasa la kwanza katika shule ya msingi Kalangalala, amekutwa amefariki dunia ikiwa ni siku sita zimepita tangu aripotiwe kupotea nyumbani alikokuwa akiishi na bibi yake katika eneo la Katoma, kata ya Kalangalala manispaa ya Geita.

Vilio na majonzi vimetawala kwa familia ya mtoto huyo aliyekuwa anaishi na bibi yake Bi.Salma Mrisho ambapo siku ya Jumatatu Septemba 29, 2025 mtoto huyo hakurudi nyumbani baada ya kumuaga Bibi yake kuwa anaenda kucheza na watoto wenzake.

Bibi huyo alipoona imefika saa mbili usiku mtoto hajarudi nyumbani alitoa taarifa kwa uongozi wa mtaa kama anavyoeleza.

Rashid Lugwisha, Daktari kutoka hospitali ya Manispaa ya Geita pamoja na Jeshi la polisi walifika eneo la tukio na kuruhusu ndugu na jamii kuendelea na taratibu za maziko kutokana na mwili wa marehemu kuharibika vibaya huku wakiendelea na uchunguzi kuwatafuta waliousika na kifo cha mtoto huyo. 

 

Chanzo: Eatv

Kuhusiana na mada hii: