Viongozi mbalimbali wakiwemo wastaafu, wafanyabiashara na watu mashuhuri jana Januari 10, 2026 walishiriki kwenye harusi ya binti wa Mdhamini na Mfadhili wa Klabu ya Yanga, Ghalib Said Mohammed, Fatma Ghalib Said Mohammed, kwenye ukumbi wa Diamond Jubilee, Dar es Salaam.
Miongoni mwa viongozi walioshiriki ni pamoja na Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Dkt. Hussein Mwinyi, Rais Mstaafu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Waziri Mkuu, Dkt. Mwigulu Nchemba na Spika wa Bunge, Mussa Azan Zungu.

Wageni wengine walioalikwa ni pamoja na Waziri Mkuu mstaafu, Kassim Majaliwa, Waziri wa Madini, Anthony Mavunde, Waziri wa Maji, Juma Aweso na Naibu Waziri wa Habari, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma almaarufu Mwana FA.
Chanzo; Global Publishers