Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Elimu, Uzazi wa Mpango si Chanzo cha Ugumba

Wataalamu wa afya wameeleza kuwa matumizi ya njia za uzazi wa mpango hayasababishi ugumba kwa mwanamke, huku wakihimiza jamii kuzingatia taarifa sahihi badala ya dhana potofu zinazoenea katika baadhi ya maeneo.

Akizungumza kuhusu suala hilo, mtaalamu wa afya ya uzazi amesema kuwa hakuna njia ya uzazi wa mpango inayosababisha mwanamke kupoteza uwezo wake wa kushika mimba kwa kudumu. Amefafanua kuwa mwili wa mwanamke hurudia katika hali yake ya kawaida mara tu anapoacha kutumia njia husika.

“Ni muhimu jamii kufahamu kuwa njia za uzazi wa mpango zimefanyiwa tafiti na kuthibitishwa kuwa salama. Mwanamke anapoamua kuacha kutumia njia hizo, uwezo wa kushika mimba hurudi kama kawaida,” alieleza mtaalamu huyo.

Aidha, wataalamu wamebainisha kuwa upotoshaji wa taarifa umekuwa ukichangia baadhi ya wanawake kushindwa kufikia huduma hizo muhimu, hali inayoweza kuathiri mipango ya familia na afya ya mama na mtoto.

Huduma za uzazi wa mpango zimeendelea kutajwa kuwa chachu ya kuboresha afya ya uzazi, kusaidia upangaji wa familia, pamoja na kuwezesha wanawake na wanandoa kufanya maamuzi sahihi kuhusu idadi na muda wa kupata watoto.

Jamii imehimizwa kutembelea vituo vya afya vilivyo karibu ili kupata ushauri wa kitaalamu na kuchagua njia inayokidhi mahitaji yao kwa usalama zaidi.

 

 

Chanzo; Crown Media

Kuhusiana na mada hii: