la Polisi Mkoa wa Ruvuma linamshikilia mwanaume mmoja ambaye jina lake limehifadhiwa, mkazi wa kijiji cha Tingi kilichopo wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma, kwa tuhuma za kumjeruhi mke wake kwa kumchoma tumboni kwa kutumia kitu chenye ncha kali.
Akizungumza kuhusu tukio hilo, Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Ruvuma, SACP Marco Chilya, amesema tukio hilo lilitokea tarehe 21 Januari 2026 majira ya saa moja usiku katika kijiji cha Tingi.
Amesema mtuhumiwa anadaiwa kumchoma mke wake baada ya kugundua kuwa alikuwa akitumia dawa za kufubaza virusi vya ukimwi (ARV) kwa siri bila kumshirikisha mume wake.
Katika tukio lingine, Kamanda Chilya amesema kuwa mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina la Catherine Kinyongile mwenye umri wa miaka 56 amefariki dunia baada ya kushambuliwa na mamba. Tukio hilo lilitokea tarehe 20 Januari 2026 majira ya saa nne usiku katika kijiji cha Ndonga, wilaya ya Nyasa mkoani Ruvuma.
Amesema marehemu alikuwa anaoga katika eneo la fukwe ya Hyetu iliyopo katika Ziwa Nyasa wakati alipokamatwa na mamba na kusababisha kifo chake. Jeshi la Polisi kwa kushirikiana na mamlaka nyingine linaendelea kuchukua tahadhari na kutoa elimu kwa wananchi wanaoishi pembezoni mwa Ziwa Nyasa kuhusu hatari ya wanyama wakali na umuhimu wa kuchukua tahadhari wakati wa kutumia maeneo ya maji.
Chanzo; Eatv