Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Matumizi Mabaya ya AI Yatajwa Chanzo cha Uhalifu

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Patrobas Katambi, amesema matumizi ya Akili Bandia (AI) ni miongoni mwa maendeleo ya kiteknolojia yasiyoepukika, lakini pia yanaweza kuwa chanzo kipya cha uhalifu endapo hayatadhibitiwa kwa umakini.

‎Akizungumza jijini Dodoma katika Kikao cha Kwanza alichofanya na Uongozi wa Juu wa Jeshi la Polisi, Maafisa na Askari, Waziri Katambi alisema Serikali imejipanga kuimarisha mifumo ya udhibiti wa uhalifu unaochochewa na maendeleo ya teknolojia.

‎Amesisitiza kuwa pamoja na manufaa ya AI katika kuharakisha maendeleo ya kijamii na kiuchumi, ipo haja kubwa ya kuhakikisha matumizi yake hayavurugi usalama wa taifa.

 

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: