Yuko Wapi Polepole ? Ndilo swali na gumzo kubwa kwa sasa nchini Tanzania baada ya kutokea taarifa ya kutoweka kwake katika mazingira ya kutatanisha siku ya Jumatatu Oktoba 6, 2025.
Polisi wamesema wameanzisha uchunguzi kuhusu madai ya kutekwa kwa mwanasiasa huyo ambaye zamani alikuwa balozi wa Tanzania nchini Cuba, kabla ya kugeuka kuwa mkosoaji mkubwa wa serikali ya Rais Samia Suluhu.
Hapo awali, polisi ilimtumia barua ya kutaka ajiwasilishe kwa uchunguzi wa makosa yanayoweza kuwa ya jinai. Taarifa ya Polisi imesema jeshi hilo bado linamsubiri.
Kumekuwa na madai ya watu kutekwa na watu wasiojulikana nchini Tanzania katika mazingira ya kutatanisha, na ambayo huwaacha jamaa na umma katika hali ya hofu.
Chanzo; Dw