Mahakama ya Wilaya Manyoni imewahukumu Mwandu Matogolo (40) na Lameck Simon (41) wakulima na wakazi wa Kijiji cha Chikola, Wilaya ya Manyoni mkoani Singida, kifungo cha miaka 30 jela na kulipa faini ya Tsh. 500,000/= kila mmoja kwa kosa la kubaka kwa kundi.
Washtakiwa walitenda kosa hilo mnamo Septemba 04, 2025, katika Kijiji cha Chikola, na walikamatwa na kufikishwa Mahakamani Septemba 17, 2025.
Hukumu hiyo imetolewa Januari 30, 2026, mbele ya Hakimu Mkazi Mfawidhi Mheshimiwa Alisile Mwankejela baada ya Mahakama kuridhishwa na ushahidi uliotolewa na upande wa Jamhuri.
Chanzo; Bongo 5