Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Taarifa Kundi la Uasi Kuibuka Mwanza Zakanushwa

Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza limetoa wito kwa wananchi kupuuza taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii zenye kichwa cha habari kinachoeleza kuwa “kundi la uasi laibuka Mwanza, Polisi waonekana mitaani.”

Kulingana na Taarifa ya Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Mwanza, Naibu Kamishna wa Polisi (DCP), Wilbrod Mutafungwa amesema taarifa hizo ni za upotoshaji zikiwa na lengo la kuleta taharuki kwa jamii, kwani wahalifu wa matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii wamekuwa wakichukua picha za askari na vitendea kazi vyao kisha kutengeneza maudhui yenye lengo la kuzua taharuki, kuchonganisha na kupandikiza chuki.

"Jeshi la Polisi linawasisitiza wananchi kuendelea kuwapuuza watu kama hao wanaosambaza taarifa zenye nia ovu na badala yake wafuatilie na kupata taarifa zenye ukweli na usahihi kutoka kwenye mamlaka zenye jukumu la kufanya hivyo." Amesema Kamanda Mutafungwa.

Aidha, Jeshi la Polisi limesema linaendelea kuwafuatilia kwa karibu watu wote wanaoandaa na kusambaza taarifa za uongo, uchonganishi na zenye kupandikiza chuki kwa jamii kwani ni kinyume cha sheria za nchi. 

 

 

Chanzo; Eatv

Kuhusiana na mada hii: