Changamoto ya mikopo imeelezwa kusababisha msongo wa mawazo kwa wanandoa wengi nchini hali ambayo imesababisha wanaume kupoteza nguvu za kiume na wanawake kukosa hisia kwa waume zao kutokana na mawazo ya madeni.
Akizungumza wakati akimnadi mgombea wa udiwani kata ya Madukani, mjumbe wa kamati ya siasa ya wilaya ya Dodoma Mjini, Chris Madaha, alisema familia nyingi zimevunjika mkoani humo kutokana na mikopo “kausha damu” ambayo imeathiri hata maisha ya kindoa.
Madaha alieleza kuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, ameliona tatizo hilo na ameahidi ndani ya siku 100 baada ya kuchaguliwa atalifanyia kazi kwa kuongeza upatikanaji wa mikopo ya asilimia 10 kwa makundi mbalimbali.
Kwa upande wake, mgombea udiwani wa kata hiyo, Profesa Davis Mwamfupe, alisema atahakikisha vijana, wanawake na watu wa makundi maalum wanapatiwa mikopo ya asilimia 10 bila kubugudhiwa.
Chanzo: Clouds Tv