Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Bweni Lateketea kwa Moto Shule ya Asha-Rose Migiro

Usiku wa kuamkia leo Jumatatu, Septemba 29, 2025, bweni moja la wanafunzi wa Shule ya Wasichana ya Asha-Rose Migiro, iliyopo Kitongoji cha Makuyuni, Wilaya ya Mwanga, limeteketea kwa moto na kusababisha hasara kubwa ya mali lakini bila kupoteza maisha ya mwanafunzi yeyote kati ya 347 waliokuwa wakilitumia bweni hilo.

Kamanda wa Jeshi la Zimamoto na Uokoaji Mkoa wa Kilimanjaro, Jeremiah Mkomagi, amesema moto huo ulilipuka ghafla wakati wanafunzi wakiwa kwenye kipindi cha prepo, jambo lililosaidia kuzuia madhara makubwa ya kibinadamu.

“Bweni hili lilikuwa likitumika na wanafunzi wa kidato cha kwanza, cha pili na cha tatu. Hakuna mwanafunzi aliyejeruhiwa kutokana na moto huu. Hata hivyo, wanafunzi 46 walipata mshtuko na kukimbizwa katika kituo cha afya cha Mwilange, ambako wanaendelea kupatiwa matibabu,” alisema Mkomagi.

Miongoni mwa mali zilizoteketea ni vitanda , magodoro, makabati ya nguo na shelfu za viatu, vyote vikiwa mali ya shule hiyo.

Kamanda Mkomagi amesema uchunguzi wa chanzo cha moto bado unaendelea, na matokeo ya awali yatawekwa wazi mara uchunguzi utakapokamilika.

 

Chanzo: Clouds Media

Kuhusiana na mada hii: