Israel imethibitisha kwamba mwili wa Mtanzania Joshua Loitu Mollel aliyeuawa na Hamas umetambuliwa baada ya kupokelewa kutoka Gaza usiku wa kuamkia Alhamis.
Mollel, aliyekuwa na umri wa miaka 21, alikuwa mwanafunzi wa mafunzo ya kilimo katika Kijiji cha ujamaa cha Kibbutz Nahal Oz karibu na mpaka wa Gaza.
Alitekwa akiwa hai na kuuawa na wapiganaji wa Hamas mnamo Oktoba 7, 2023, kisha mwili wake kupelekwa Gaza. Aliwasili katika kijiji hicho siku 19 tu kabla ya shambulio, baada ya kumaliza chuo cha kilimo nchini Tanzania, akitaka kupata uzoefu katika sekta ya kilimo.
Chanzo; Dw