Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Chaba, Dudukwe AI Yawatia Hofu, Yawachoresha Kivingine

Watu wa jamii ya wawindaji na wakusanya matunda wa kabila Wahadzabe wanaoishi eneo la Mang’ola wilayani Karatu wamepatwa na hofu kubwa ya matumizi ya teknolojia ya akili unde ambayo kwa muda sasa imekuwa ikitumiwa na baadhi ya watengeneza maudhui wakiwaonyesha kuishi maisha tofauti na asili yao.

Vijana wawili maarufu kwa majina ya Chaba na Dudukwe wamekuwa waathirika wakubwa wa kadhia hiyo na ITV imewatembelea na kusikia mtazamo wao.

Pamoja na matumizi ya akili unde lakini pia upo utaratibu unaotumika kwa wageni wanaokwenda kuwatembelea watu hao kuwapelekea vitu ambavyo ni tofauti na mahitaji ya asili yao.

ITV ikazungumza na Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amos Makala kujua msimamo wa Serikali juu ya ulinzi wa haki za watu wa jamii hiyo.

 

 

Chanzo; Itv

Kuhusiana na mada hii: