Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Wakandarasi Wanaohamisha Fedha za Miradi Waonywa

vWaziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. Mwigulu Nchemba, amewataka wakandarasi nchini kutekeleza miradi kulingana na fedha wanazopokea, akisisitiza kuwa baadhi yao wamekuwa wakitumia fedha za miradi kwenye shughuli zisizohusika.

Dkt. Nchemba alitoa rai hiyo wakati wa hafla ya uwekaji jiwe la msingi la mradi wa kituo cha kupoza na kusambaza umeme cha msongo wa kilovoti 132/33 cha Mkata, kilichopo wilayani Handeni mkoani Tanga. Alieleza kuwa fedha zinazotolewa na Serikali zinapaswa kuendana moja kwa moja na kazi iliyotekelezwa kwenye mradi husika.

Aliongeza kuwa Serikali imebaini kuwepo kwa baadhi ya wakandarasi wanaochezea fedha kwa kuzielekeza kwenye miradi mingine au kuzihamishia kwenye akaunti zilizo nje ya nchi, hali inayokwenda kinyume na masharti ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Alisisitiza kuwa ni lazima thamani ya fedha ionekane wazi katika kazi inayofanyika.

Mradi wa ujenzi wa kituo cha kupoza umeme cha Mkata unatekelezwa na kampuni ya TBEA kutoka China. Ujenzi ulianza Agosti 23, 2023 na unatarajiwa kukamilika Machi 10, 2026 kwa gharama ya shilingi bilioni 44.14.

Kukamilika kwa mradi huo kunatarajiwa kuboresha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika wilaya za Handeni na Kilindi, kuongeza huduma ya umeme katika maeneo ya migodi ya graphite, pamoja na kuongeza mapato ya shirika la umeme kutokana na ongezeko la wateja wapya watakaounganishwa baada ya mradi kukamilika.

 

 

Chanzo; Wasafi Media

Kuhusiana na mada hii: