Waziri wa Mambo ya Ndani, George Simbachawene, amesema Serikali imeanza mazungumzo yenye lengo la kuboresha masilahi, ikiwemo makazi na posho, kwa askari wote wa Jeshi la Polisi nchini.
Amesema kuwa hatua hiyo itawezesha kuboresha mazingira ya kazi pamoja na kuwaongezea ujuzi na utaalamu, ili kuendana na mazingira ya sasa ya kukabiliana na uhalifu, ukiwemo ule wa mtandaoni.
Waziri Simbachawene ameeleza hayo leo, Jumanne, Januari 6, 2026, alipozungumza na maofisa, wakaguzi, askari wa Renk na faili wa makao makuu ya Polisi Zanzibar, pamoja na mikoa mitatu ya Unguja.
Chanzo; Mwananchi