Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mvua Yaua Watatu Songwe, AkiwemoMwanafunzi wa Shule ya Msingi

Watu watatu akiwamo mwanafunzi wa darasa la pili, wamefariki dunia kufuatia mvua zinazoendelea katika maeneo mbalimbali mkoani Songwe huku Jeshi la Polisi likiwakumbusha wananchi kuchukua tahadhari.

Taarifa iliyotolewa na jeshi hilo Februari 21, 2026 imeeleza kuwa matukio ya vifo, hivyo yametokea Februari 20, 2026 katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo kufuatia mvua zinazoendelea likiwataka wananchi kuchukua tahadhari.

Taarifa hiyo imeeleza kuwa tukio la kwanza lilitokea saa 10 jioni katika Kijiji cha Ssenga, Kata ya Halungu wilayani Mbozi ambapo mtu mmoja, Said Kamwela (62) alifariki dunia kwa kuzama kwenye maji.

Imefafanua kuwa Kamwela alifariki dunia wakati akioga kwenye mto Halumu kutokana na kina kikubwa cha maji kilichosababishwa na mvua iliyonyesha na kusababisha kifo chake.

Tukio lingine lilimuhusisha mwanafunzi wa darasa la pili katika Shule ya Msingi Migombani, Janeth Tarimo baada ya kuteleza na kutumbukia katika korongo lililokuwa na maji mengi alipokuwa akitoka shuleni kisha kusombwa na maji hayo, saa 10 jioni huko Kaloleni wilayani Momba.

Pia, imeeleza kuwa saa 1 usiku, mtu mmoja ambaye hajafahamika jina lake anayekadiriwa kuwa na miaka 30, alifariki dunia baada ya kuteleza na kutumbukia kwenye korongo lililokuwa likitiririsha maji kutokana na mvua zinazoendelea.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: