Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Mashahidi 177 Kesi ya “Dk. Manguruwe”

Mashahidi 117 wanatarajiwa kutoa ushahidi wao mahakamani katika kesi ya kuendesha biashara ya upatu inayomkabili Mkurugenzi wa Kampuni ya Vanilla International Ltd, Simon Mkondya, maarufu Dk Manguruwe, na mwenzake.

Pia, upande wa Jamhuri unatarajia kuwa na vielelezo zaidi ya 100. Mkondya na mwenzake, Rweyemamu John, ambaye ni meneja na mkaguzi wa fedha wa kampuni hiyo, wanakabiliwa na mashtaka 126 yakiwemo ya kuendesha biashara ya upatu na utakatishaji fedha, yanalomkabili Mkondya pekee.

John, yeye yupo nje kwa dhamana baada ya kuiomba dhamana Mahakama Kuu na hana mashtaka ya kutakatisha fedha.

Mashahidi hao wanatarajia kutoa ushahidi wao katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, baada ya Mkurugenzi wa Mashtaka nchini (DPP) kuwasilisha kibali cha kuruhusu mahakama hiyo kusikiliza kesi hiyo ya uhujumu uchumi.

Hatua hiyo inatokana na upelelezi wa kesi hiyo kukamilika katika Mahakama ya mkoa wa Dar es Salaam.

Haya yameelezwa na Wakili wa Serikali, Titus Aron, leo Jumatatu, Januari 5, 2026, wakati kesi hiyo ilipoitwa kwa ajili ya Jamhuri kuwasomea hoja za awali (PH) kwa washtakiwa hao.

 

 

 

Chanzo; Mwananchi

Kuhusiana na mada hii: