Mwanafunzi wa shahada ya sheria Chuo Kikuu cha Mzumbe Tawi la Mbeya, Shyrose Mahande (21), ameuawa kikatili baada ya kutekwa na watu wasiojulikana.
Taarifa zinaeleza kuwa Mahande alitekwa Jumamosi na watu wasiojulikana walimtumia baba yake mzazi, Dkt. Mabula Mahande, video fupi zikimuonyesha akiteswa, huku wakidai kiasi cha fedha ili kumuachia huru.
Kwa masikitiko makubwa, Mahande amepatikana akiwa ameuawa kwa kuchomwa moto kwenye vibanda vya biashara eneo la Nane Nane mkoani Mbeya.
Vyombo vya usalama vinaendelea na uchunguzi wa kina kubaini waliotekeleza tukio hilo na hatua za kisheria kuchukuliwa.
Chanzo; Global Publishers