Vituo 38 vya mafuta vimeathiriwa nchini na maandamano Oktoba 29, mwaka huu, huku wafanyakazi takribani 300 wakikosa kazi kwa sasa, kwa kupatiwa likizo bila malipo.
Miji iliyoathiriwa ni pamoja na Dar es salaam, Arusha, Mwanza na Mbeya, pia Shinyanga, Geita, Songwe, Ruvuma, Mara, Dodoma, Kilimanjaro na Iringa kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Jeshi la Polisi nchini.
Mkurugenzi wa Uendeshaji wa Lake Oil Group, Stephen Mtemi, ameelezea hayo leo, na namna walivyoathiriwa, huku akitoa pole pia kwa wananchi walioathirika kwa namna moja au nyingine.
Chanzo; Nipashe