Waziri Mkuu wa Dkt. Mwigulu Nchemba ametoa onyo kwa wakandarasi wanaoshindwa kuwalipa vibarua kwa wakati, ilhali Serikali tayari imeshawalipa fedha za miradi husika.
Akizungumza leo katika hafla ya uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa mabweni ya wanafunzi katika Taasisi ya Afrika ya Sayansi na Teknolojia ya Nelson Mandela, Kampasi ya Tengeru mkoani Arusha, Dkt. Mwigulu amesema Serikali haitavumilia tabia ya kuwakandamiza wafanyakazi kwa kucheleweshwa malipo yao.
Chanzo; Crown Media