Wakati watu walikuwa wanaona kipindi cha Corona “Covid19” kama kipindi kigumu katika kufanikisha mambo ikiwemo biashara na hata baadhi ya kazi kama ilivyokuwa, Sallam Sk yeye anaenda tofauti na usemi huo kupitia msanii wao, ambaye kwasasa anaweza kuwa sehemu ya Top 5 ya wasanii wanawake bora Tanzania.
“Zuchu aliletwa na mama yake, wakati wa Corona nimelazwa Temeke, mimi na laizer na mtoto wa Mbowe. Tukawa tumeongea Diamond, akasema tumtoe Zuchu, laizer alikuwa kule kule akawa anafanya mixing.” - Sallam Sk
“Huu ndio wakati muafaka sababu ananyimbo zake za slow nikasema nikitoka tutafanya launch. Corona ilivyokuwa imetulia tukasema huu ndio wakati muafaka wakutoka Zuchu, aishukuru Corona.” - Sallam Sk
Dozen akadai Zuchu alitoka wakati mgumu, majibu ya Sallam Sk “Sio wakati mgumu sababu nyimbo nyingi zilikuwa za slow ndio maana zilishikia sana sababu ilikuwa sio muda wa kupart watu wanapitia magumu nadhani ilikuwa right time.”
Zaidi, amekanusha kummiliki Zuchu kama msanii wake ndani ya WCB, kama ilivyofahamika hapo awali kuwa Mbosso ni msanii wa Babu Tale, Rayvanny ni msanii wa Mkubwa Fella.
Chanzo; Tanzania Journal