Search

Saved articles

You have not yet added any article to your bookmarks!

Browse articles

GDPR Compliance

We use cookies to ensure you get the best experience on our website. By continuing to use our site, you accept our use of cookies, Privacy Policy, and Terms of Service.

Roma Amjibu Nikki Mbishi Kuhusu Ushamba na Show

Msanii wa Hip-hop nchini, Roma Mkatoliki amemjia juu msanii mwenzake, Nikki Mbishi baada ya kumdisi kwenye mahojiano aliyofanya akidai ni mshamba, hajawahi kuandaa shoo yake binafsi akapata mashabiki.

Kupitia ukursa wake wa Instagram, Mkatoliki amechapisha video za uthibisho wa shoo alizoandaa na kupafomu. Huku akiondoka na kijiji cha mashabiki, hatahivyo ameandika na kumfafanulia Nikki, nini maana ya kuandaa shoo binafsi.

"NIKKI kuandaa show yako maana yake sio msanii ubebe sound na machuma ya stage uende ukayafunge mwenyewe ukumbuni. Na ukae na mlangoni kuchukua kiingilio NO, hiyo siyo maana ya kuandaa show.

"Kuandaa show yako maana yake ni event inaandaliwa kwa jina lako ama wewe ndio unakuwa main act katika hiyo event. And Yes, nimeshafanya hivyo sana! Google, ingia YouTube utakutana nazo," ameandika Roma.

Roma ameendelea akisema zaidi ya miaka 18 katika gemu ya muziki hakuna jiji, mkoa, wilaya ndani ya Tanzania hajafika kufanya shoo.

"Nina miaka 18 kwenye game, miaka yote hiyo hakuna jiji, mkoa, wilaya, kijiji ndani ya Tanzania sijafika kufanya show. Hakuna Nikki! Kusini, Kaskazini, Pwani, Kanda ya Ziwa, Central, Nyanda za Juu Kusini, Magharibi, Zanzibar hadi Mafia nimefika.

"Na sehemu zote hizo sio mara moja, ni zaidi ya mara 5 iende irudi kila mwaka! Na ni kwa show zangu mwenyewe ONE MAN AAAA!! Na sio tamasha la wasanii wengi!," ameandika Roma.

Kwa majibu hayo Mkatoliki amemtaka Nikki Mbishi aoneshe shoo zake mbili ambazo ziliandaliwa kwa jina lake. Hata hivyo amesema shoo anazofanya Nikki sio Corporate kama anavyodai bali ni Chaka to Chaka ambazo kwa upande wake alifanya shoo hizo miaka ya 2010 hadi 2013.

"Nadhani nimekujibu kwa mifano hai (Facts) Mambo kwa ushahidi. Haya ukimaliza kutazama please naomba na wewe tuonyeshe shows zako binafsi. Mbili tu sitaki nyingi! Tena usituonyeshe hata video NO, epuka aibu ndogo ndogo za kuonyesha idadi ya watu uliopata.

 

Chanzo: Mwananchi Scoop

Kuhusiana na mada hii: